image

BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni limevunjwa rasmi juzi kufuatia serikali kuigawa halmashauri ya manispaa hiyo kuwa mbili.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, alisema jana kuwa amelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na kuwapo kwa halmashauri mpya ya Ubungo.

Alisema alivunja baraza hilo baada ya kumalizika kwa kikao cha kawaida na kwamba uchaguzi mpya wa Meya unatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia jana na kwamba meya wa sasa, Boniface Jacob (Chadema) amepoteza nafasi yake hiyo akisubiri uchaguzi.

Kagurumjuli alisema baada ya wilaya hiyo kugawanywa, hivi sasa kila wilaya ina mkurugenzi wake, wakuu wa wilaya wake na makatibu tawala wao.

Advertisements