Mweneyekiti wa muda wa CUF Julius Mtatiro amedai aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Ibrahim Lipumba alilipwa fedha nyingi sana na CCM lakini walikuwa wamekaa kimya tu ili kumstahi.

Amesema Lipumba amenunua ghorofa la milioni 900 amenunua depot sheli, pia alichangisha milioni 280 na wabunge wa CUF kwenye akaunti yake binafsi kwa ajili ya kugombea urais lakini alitokomea na fedha hizo alipoacha azma yake ya kugombea urais na kujiuzulu uenyekiti

image
Ibrahim lipumba

Mtatiro amesema amebidi kutoa siri zake na atatoa nyingine zaidi kwa kuwa walikuwa wanamuheshimu kama mwanachama wao na mwenyekiti wao wa muda mrefu lakini alipoanza kuteka na kutishia kuua wanachama wa CUF wamepoteza heshima waliyokuwa nayo kwake

Advertisements