SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limepata pigo katika mgogoro wake wa muda mrefu wa kisheria juu ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL),

Ambapo sasa limetakiwa kuilipa benki ya Standard Chartered Bank-Hong Kong (SCB-HK) dola za Marekani milioni 148.4 (zaidi ya Sh. bilioni 320).

tanesco images

Pigo hilo limekuja wiki iliyopita baada ya Baraza la Usuluhishi la Benki ya Dunia kutoa hukumu ya kulipwa kwa kiasi hicho cha fedha ambacho kinajumuisha na riba ya deni la tozo ya uwekezaji.

Uamuzi huo umekuja miaka mitatu tangu serikali iruhusu kitatanishi kufanyika kwa malipo ya dola milioni 200 (sawa na Sh. bilioni 440) kutoka katika akaunti ya Tegeta escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda kwa kampuni ya Harbinder Singh Sethi ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP).

Advertisements