Hakuna kitu kizuri kama michezo atakwambia nani kuna starehe nzuri duniani kama hii ya kuona wanamume wakitoana jasho uwanjani haswa wakiwa na udamwbi dambwi pale katikati ya uwanja, raha sana angalia Barcelona ama Arsenal ukitaka mpira wa namna hiyo utasuuzika na moyo wako.

images

Leo hii nakuletea misemo mbalimbali ya mchezaji nyota Paul Pogba huko mitaani tena misemo hiyo imetoka kwa mashabiki wa Tanzania baada ya kuanza vibaya kwa mchezaji huyo japo anastahili apewe muda.

NITAKUPA POGBA

Mtaani ukisikia watu wanasema neno hili ujue unauziwa kitu kibaya ama kitendo unachofanyiwa cha utapeli kwa kuwa pesa aliyonunuliwa ni ndefu sasa wanachukulia hapo ikiwa kama kituko fulani mtaani kwa Tanzania huwa tuna mambo mengi sana.

images-1

JUVENTUS TAPELI MKUBWA DUNIANI

Hapa unaweza kucheka jinsi wabongo wanavyojua kutania watu, baada ya Paul Pogba kununuliwa kwa kiasi cha pauni milioni 89 sasa wabongo wamelipuka na kusema kuwa Juventus ni matapeli wamewatapeli Manchester United wakati mchezaji huyo alikuwa na thamani kidogo.

NIPE CHAKULA NITAKUPA POGBA KESHO

Hili neno nimelisikia katika mgahawa mmoja huku Kinondoni wakimwambia mama muuzaji kuwa awape chakula kisha hela kesho ina maana neno Pogba linatumika kama utapeli pia huku mtaani, kwa kweli maneno ni mengi mno huku mtaani yanachekesha.

NIONAVYO MIMI

Bado Paul Pogba ananafasi ya kufanya vizuri zaidi kwani hajapotea sana, labda aina ya wachezaji anaowapanga nao mzee Mourinho ndio kikwazo, aina ya wachezaji wa aina yake wote wako na mpira wa taratibu mfano Fellain hivyo si muda sahihi wa kumlumu, unakumbuka ile ya Gareth Bale ? Wakati anatua Madrid watu walimponda sana ilichukua takribani miezi 9 hadi kukaa sawa, hivyo tumpe muda Pogba naamini atafanya makuu.

download

Advertisements