Baada ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini Slovenia, Aleksander Ceferin kushinda wadhifa wa kuwa Rais wa UEFA kwa kura 42 kati ya 55 akichukua mikoba ya Michael Platini hatimaye amezungumzia mipango yake.

Katika mahojiano na Gazeti la Hispania la Marca Ceferin, amesema moja ya mipango yake mikubwa ni kupitia upya sheria iliyopitishwa na kamati ya utendaji ya UEFA kuhusu kuzipa nchi za Italia, Hispania, Uingereza na Ujerumani nafasi nne za kuingiza vilabu moja kwa moja kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

image
Lionel messi

Ceferin pia aliulizwa kuhusu ushindani wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo alisema ni ushindani mzuri kwenye soka na unasaidia kuwafanya wengine wajitume huku akisisitiza kuwa wachezaji hao wanatofautiana na kila mmoja ana ubora wake.

image
CR7

Ronaldo anajitihada binafsi na nguvu pamoja na nia ya kufanya vizuri huku Messi akiwa ni zaidi ya msanii. “Ronaldo is pure power, strength, determination whereas Messi is more of an artist”.

Advertisements