Kiungo wa Manchester City Yaya Toure mwenye miaka 33, ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa.

Toure aliichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza mwaka 2004, na baada ya miaka 10 yaani mwaka 2014 alikabidhiwa unahodha kutoka kwa Didier Drogba.

image

Mwaka 2015 aliiongoza Timu ya Taifa ya Ivory Cost kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza tangu 1992. Hadi anastaafu soka la kimataifa tayari Yaya Toure ameichezea Ivory Coast mara 113.

image

Wakati huohuo Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hatomchezesha Yaya Toure mpaka kwanza aombe radhi kufuatia matamshi yaliyotolewa na wakala wake.

Advertisements