Baada ya kuona mechi mbili ambazo Granit Xhaka amecheza na kuonesha umahiri wake wa kufunga magoli ya mbali kwa mashuti makali ambayo tulikosa kuyaona ligi kuu England tangu Gerrard na Lampard waondoke katika ligi hiyo.

image

Xhaka anaonekana anaweza kufanya kitu pale Arsenal haswa kwa pasi zake za juu ambazo zinaona wapi zinaelekea huku akiwa na nguvu kuzuia mashambulizi kwa adui. Kwa mechi kadhaa amabazo amecheza ameonekana msaada mkubwa Arsenal pongezi zimfikie Arsene Wenger kwa kuona kipaji cha Xhaka.

Nimeona mchezaji huyu anaweza kuiokoa Arsenal haswa kuamua matokeo, mpira wa washika bunduki hao unafahamika kwa kufunga wakiwa ndani ya Box la 18 kwa adui. Xhaka ambae amenunuliwa pauni milioni 30 kutoka katika ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga kutoka pale Borussia Mönchengladbach.

Mchezaji huyu anaweza kupiga mashuti makali ambayo ni silaha kubwa kwa timu hiyo kumbuka wiki hii Arsenal wanawakaribisha watani wao Chelsea katika dimba la Emirate.

Advertisements